Klabu ya Manchester United ipo tayari kupokea zaidi ya euro milioni 40 ili kuachana na Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini England Jadon Sancho, kwa mujibu wa ripoti.

Sancho alijiunga na Borussia Dortmund kwa mkopo Januari baada ya kutofautiana na kocha Erik ten Hag, lakini mpango huo haujumuishi chaguo la uhamisho wa kudumu na hivyo winga huyo kwa sasa anatarajiwa kurejea Old Trafford msimu huu wa majira ya joto.

Hata hivyo, iwapo Erik ten Hag ataendelea kuinoa United, Sancho huenda akaondoka jumla na Sky Sport inaeleza kuwa anataka kubaki na Dortmund, ambayo pia inataka kufanya makubaliano na United.

Kikwazo kikuu kwa Dortmund ni gharama yake, kwani United ililipa Pauni Milioni 73 kumsajili Sancho mwaka 2021, na hivyo kumsainisha mkataba mnono ambao unatarajiwa kumalizika msimu wa majira ya joto wa 2025, na wanatafuta karibu nusu ya kiasi hicho ili kumuuza Sancho.

Kutumia fedha za aina hiyo kwa mchezaji mmoja itakuwa ngumu sana kwa Dortmund, ambayo pia haiwezi kutoa popote karibu na aina sawa ya mshahara anayopokea Sancho kwa sasa.

Mkataba wa kudumu bado haujatolewa lakini mazungumzo kati ya Dortmund na United bado yako mbali sana na azimio hilo.

Sancho amefunga mabao mawili na pasi mbili za mabao katika mechi 11 alizocheza hadi sasa akiwa na Dortmund, ambapo viongozi wa klabu hiyo wamekiri wazi kuwa hawakutarajia mengi kutoka kwa mchezaji huyo ambaye alikaa nje ya uwanja kwa miezi minne kabla ya kujiunga nao.

PSG imedhamiria kwa Victor Osimhen

Mustakabali wa Sancho unaweza kuunganishwa na winga mwingine wa Dortmund, Donyell Malen.

Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 25, amekuwa katika kiwango bora na akiwa amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake, anaaminika kuwa na nia ya kuhamia Ligi Kuu England.

Mha. Kasekenya: Magari ya Serikali mwisho saa 12 Barabarani
Polisi afyatua risasi kukwepa deni la Pombe