Watumishi wa Umma wanaotumia magari ya Serikali kwa matumizi binafsi sasa watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria ambapo Maafisa Masuuli wote wamekumbushwa kusimamia maelekezo hayo.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mha. Godfrey Kasekenya ameyasema hayo hii leo Aprili 8, 2024 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Arumeru Magharibi, Noah Saputu aliyetaka kujua ni lini Serikali itazuia kupaki magari ya Serikali sehemu za starehe baada ya masaa ya kazi.

“Serikali kupitia Waraka wa Rais Na. 1 wa Mwaka 1998 kuhusu hatua za kubana matumizi ya Serikali, ilielekezwa kuwa magari yote ya Serikali yanatakiwa kuwa yameegeshwa sehemu zilizotengwa kwa ajili hiyo ifikapo saa 12.00 jioni bila kukosa vinginevyo kiwepo kibali rasmi kinachoruhusu gari la Serikali kuwepo barabarani baada saa 12.00 jioni,”amesema.

Amesema, Serikali kupitia Kanuni J.21 ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za Mwaka 2009 imezuia Watumishi wa Umma kutumia magari ya Serikali kwa matumizi binafsi, hivyo, mtumishi anayekwenda kinyume na maelekezo hayo anatakiwa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu.

Madaktari mnapenda pesa, Mungu atawaadhibu - Mbunge
Bei ya Sancho yaanikwa hadharani