Serikali imeanza mchakato wa kumaliza mgogoro wa ardhi unaoendeleo kati ya Viongozi wa Kimila (Machifu) na Taasisi ya Utafiti ya Kilimo (TARI) katika eneo la Chuo cha kilimo Uyole Jijini Mbeya.

Kwa niaba ya Serikali Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amekutana na pande zote mbili, Machifu na wawakilishi kutoka TARI kisha kusikiliza hoja za pande hizo mbili.

Machifu wanadai eneo la hekari nane walilotengewa sio eneo sahihi bali eneo lenye makaburi ya Viongozi wao wa kimila waliofariki miaka kadhaa iliyopita ndilo wanalopaswa kukabidhiwa.

Kwa upande wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI, wanadai eneo walilowapatia machifu ni eneo sahihi ambalo linawatosha kufanya shughuli zao za kimila na kwamba gharama zimetumika kuweka uzio kwa ajili ya kulitambua eneo hilo ambalo halitotumika kwa ajili ya shughuli za Kilimo.

Baada yq kusikiliza pande hizo mbili, Malisa ametaka kuundwa kwa kamati itakayojumuisha baadhi ya watu kutoka upande wa machifu na upande wa TARI kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya kulitafutia ufumbuzi suala hilo haraka iwezekanavyo.

Aidha, Malisa pia amezitaka pande zote mbili kuwa watulivu kwa kipndi hiki ambacho inatafutwa suluhu ya mgogoro huo na kusimamisha shughuli za kimila na kilimo katika eneo hilo mpaka pale ambapo majibu yake yatapatikana siku za hivi karibuni.

Dorice: Asilimia 90 ya Wastaafu hupoteza fedha za mafao
Dkt. Biteko amtembelea RC Mstaafu Mashishanga