Scolastica Msewa – Dar es Salaam.

Asilimia 90 ya Wastaafu nchini wamekuwa wakipoteza fedha zao za mafao kwasababu ya kuwekeza fedha zao wakiwa hawana elimu ya uwekezaji wa akiba na kuongeza mitaji yao ambayo huishia kupata hasara.

Hayo yamesemwa na Afisa Masoko wa UTT, Dorice Mlenge katika makongamano ya Women Ubuntu Tanzania lililoandaliwa na Mkurugenzi wa umoja wa Wanawake Wajasiriamali Tanzania Dkt. Angella Gloria Bondo.

Amesema, Wafanyabiashara na Wafanyakazi Vijana wanatakiwa kuanza kuwekeza akiba kadri wanavyopata ili iwasaidie kupata uzoefu badala ya kuwekeza fedha zao uzeeni.

“Wengi huamini wanaoweza kuweka akiba ni wale wenye kiwango kikubwa cha fedha au mpaka apate fedha nyingi ndipo aweze kuweka akiba dhana ambayo sio kweli kwani mwenye kiwango kidogo anauwezo wa kuweka akiba ili uweze kuongeza kipato chake pia,” alisema.

Aidha, Dorice ameomba wenye uelewa wa uwekezaji wa akiba kuwaelewesha wenzao kuweka akiba kwa ajili ya maisha yao ya baadae ili wakati wa uzeeni waweze kujipanga kimatumizi.

Awali, Mkurugenzi na Mwanzilishi wa kuwajengea uwezo Wanawake wafanyabiashara na Ma-MC Dkt. Angela Bondo amesema ni mwaka wa nne Sasa amekuwa akiwakusanya Wanawake na kuwajengea uwezo wa kufanya shughuli zao ili wapate tija katika jitihada zao za Kila siku.

Katika kongamano hilo, Wanawake wamejengewa uwezo kuhusu kutangaza biashara zaon jinsi ya kuwa mjasiriamali hodari na kufanyiwa maombi, ili Wanawake wawe na nguvu ya kiroho bila kujali dini wala dhehebu la mtu.

TARURA yakamilisha ujenzi Daraja la Chuma Mto Lwipa
Mgogoro wa ardhi Machifu, TARI: Malisa aunda kamati