Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema linao wajibu wakisheria wa kuwalinda raia na mali zao huku likibainisha kuwa limepokea maelekezo ya Mwenyekiti wa Ulinzi, Paul Makonda aliyoyatoa hivi karibuni.

Kauli hiyo, imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha SACP, Justine Masejo kufuatia maagizo ya Mkuu wa Mkoa huo ambapo alilitaka Jeshi la Polisi Mkoani humo kuimarisha ulinzi na usalama, ili kuwezesha biashara na shughuli nyingine za utalii kufanyika kwa ndani ya saa 24.

Amesema kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wameendelea kufunga kamera na taa kwenye maeneo yaliyokuwa na wingi wa matukio ya kiuhalifu ili kusaidia kubaini uhalifu na wahalifu wa katikati ya Jiji la Arusha na Mkoa huo ambao ni kitovu cha Utali hapa Nchini.

Aidha, Kamanda Masejo amebainisha kuwa lengo ni kuhakikisha mkoa mzima unakuwa na Kamera katika maeneo yote ili kusaidia katika doria na ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

Amehimiza suala la Maadili kwenye ngazi za familia na kuwalea vyema vijana ambao wana hofu ya Mungu ili kusaidia katika kupunguza matukio ya kiuhalifu katika jamii.

Ndumbaro: Tunajikita ujenzi wa viwanja AFCON 2027
Mikel Arteta kumrudisha Gabriel Heinze EPL