Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto Duniani – UNICEF, limetoa msaada wa vifaa vya Shule za msingi na Sekondari kwa Shule zilizoathirika na mafuriko katika Wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani ambapo Wanafunzi 1040 na Walimu vyenye thamani ya Dola 9586.20 .

Mkuu wa kitengo cha Elimu Maalumu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Magreth Matonya alikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge ambaye aliwakirishwa na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Meja Edward Gowele alisema vifaa vilivyotolewa ni kwa ajili ya Shule 14 zilizoathirika na mafuriko kwa Wilaya za Rufiji na Kibiti.

Amesema, msaada huo utapelekwa kwenye Shule hizo ambazo maji ya Mto Rufiji yamejaa na Wanafunzi hawawezi kuendelea na masomo na vifaa vyao vimeharibika kwa namna Moja au nyingine na mafuriko hayo yanayoendelea wilayani humo.

Dkt. Matonya alitaja aina ya vifaa hivyo vya Shule vilivyoletwa kuwa ni pamoja na mahema ya kutengeneza madarasa 4, vifaa vya kusomea Wanafunzi, vifaa vya kufundishia kwa Walimu, vifaa vya michezo na vifaa vya Wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Alisema katika mahema hayo matatu yatapelekwa kwaajili Shule 7 zilizofungwa wilaya ya Rufiji na hema moja litakabidhiwa kwaajili ya Shule zilizofungwa wilayani Kibiti.

Akipokea Msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowele alishukuru UNICEF kwa msaada huo na kusema Wilaya za Rufiji na Kibiti ina shule 23 zilizoathirika na mafuriko hayo huku shule 14 zimefungwa kwa athari za mafuriko hayo kwa Wilaya zote mbili.

Van Dijk: Tunapaswa kusahau na kusonga mbele
MALIMWENGU: Bibi wa miaka 97 apewa talaka kwa kuchepuka