Wahariri wa gazeti la Mawio lililofungiwa maisha na serikali, Jabir Idrisa na Saimon Mkina , jana walijisalimisha katika kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam kufuatia taarifa zilizotolewa na jeshi hilo kuwa wanawatafuta bila mafanikio.

Mbali na wahariri hao, wengine waliofika katika kituo hicho kwa kesi ya Mawio ni mwanasheria wa gazeti hilo, Frederick Kihwelo, Saed Kubenea (Mkurugenzi wa kampuni ya Halihalisi Publishers), Ansbert Ngurumo aliyekuwa mhariri mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.

Kubenea alieleza kuwa alifika katika kituo hicho cha polisi kwa kuwa mmoja kati ya wafanyakazi wake pia alikuwa mikononi mwa polisi.

Wahariri hao walihojiwa na jeshi la polisi katika ofisi ya Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro kuanzia majira ya saa 8:59 mchana hadi saaa 12: 42 jioni.

Awali, kamanda Siro aliwataka wahariri hao kujisalimisha polisi kwa madai kuwa wameandika habari zenye utata na za uchochezi. Alisema kuwa Polisi inataka kuwahoji kuhusu undani na ukweli wa habari walizokuwa wanaandika.

Naye mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalome Kibanda alileza kuwa aliwasindikiza waharirir hao polisi ili kufahamu kinachoendelea haswa. Kibanda pia aligusia mpango na msimamo wa Jukwaa la Wahariri kutokubali kufanya kazi na waziri wa habari, utamaduni, michezo na wasanii, Nape Nnauye.

“Sisi Jukwaa la wahariri hatukubali kufanya kazi na waziri wa aina hii na tutatoa tamko letu, ngojeeni,” alisema Kibanda.

Rekodi: Bibi wa miaka 86 avunja rekodi ya dunia kwa kupanda mlima kilimanjaro hadi kileleni
Magwiji wa Dawa za Kulevya wanaswa na serikali ya Magufuli