Serikali ya Zimbabwe imemburuza mahakamani afisa wa Polisi aliyesema kuwa Rais Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 92 ni mzee sana kuendelea kuwa kiongozi wa taifa hilo.

Afisa huyo aliyetajwa kwa jina la Thomas Joseph Mloyi pia anakabiriwa na kosa lingine akituhumiwa kumuita mke wa Rais Mugabe, Bi. Grace kuwa ni kahaba.

Afisa huyo aliachiwa kwa dhamana ya shilingi za Tanzania laki mbili na anatarajiwa kurudi mahakamani hapo Machi 15 mwaka huu.

Hivi karibuni, Rais Mugabe alisisitiza kuwa bado ana nguvu na hata akatania kuwa anaweza kumpiga konde mtu na konde hilo likampeleka chini.

Chanzo: BCC

Man Utd Yashindwa Kufurukuta Anfield
Picha: Huyu ndiye msanii wa kike anayemiliki 'gari' wa gharama zaidi Tanzania