Serikali imeyafutia usajili Magazeti 473 kwasababu ya kutochapishwa kwa muda wa miaka mitatu mfululizo. Magazeti hayo yamefutiwa usajili kupitia tangazo lililochapishwa katika gazeti la serikali lenye namba 195.

Akiongea na Waandishi wa habari mapema leo Waziri wa habari utamaduni na michezo, Nape Nnauye amesema Magazeti hayo hayataruhusiwa kuchapishwa au kusambazwa kwa njia ya nakala ngumu au kielektroniki na ikiwa mmiliki wa gazeti lililofutiwa usajili angependa kuendelea na biashara milango iko wazi kwa ajili ya kuwasilisha maombi mapya ya usajili kwa kufuata taratibu zilizopo.

Kwa mujibu wa takwimu za ofisi ya msajili wa magazeti, nchi ya Tanzania inayo magazeti na majarida 881 yaliyosajiliwa kisheria.

BreakingNews: Msafara wa Waziri Mwakyembe Wapata Ajali, Geita
Jurgen Klopp Amfukuza Super Mario Barwuah Balotelli