Mwandishi  wa habari ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Mogadishu nchini Somalia baada ya watu waliokuwa na silaha wakiwa kwenye pikipiki kumfyatulia risasi Abdi Asis Mohamed Ali alipokuwa akirudi nyumbani kwake akitokea kazini.

Mwandishi  huyo ambaye alikuwa anafanya kazi kwenye Radio Shebelle kwa miaka kadhaa alipigwa risasi na watu wawili wenye silaha wakiwa na pikipiki mjini Mogadishu na kupoteza maisha.

Uongozi wa Redio aliyokuwa akifanyia kazi umethibitisha kifo chake na kusema kuwa watu wenye silaha walitoweka kwenye eneo la tukio mara baada ya kutekeleza shambulio hilo, hii si mara ya kwanza kwa waandishi wa habari wa Redio Shabele kuuawa kwa kupigwa risasi nchini Somalia.

Umoja wa Mataifa hivi karibuni ulitoa ripoti yake ikiiorodhesha Somalia kuwa ni miongoni mwa nchi hatari kwa waandishi wa habari kufanya kazi zao nchini humo, ripoti hiyo ilisema kati ya mwezi agosti mwaka 2012 mpaka june 2016, waandishi wa habari 30 waliuawa ,  na karibu waandishi wa habari 120 wamekamatwa na wanashikiliwa nchini humo.

CUF wamfukuza rasmi Profesa Lipumba
Video: Zoezi la upandaji miti ni endelevu Wilaya ya Ilala - DC Mjema