Imefahamika kuwa Mshambuliaji kutoka nchini Argentina na klabu ya Barcelona, Sergio Arguero atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu, kutokana na kusumbuliwa na tatizo la moyo.

Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa klabuni hapo akitokea Manchester City inayoshiriki Ligi Kuu ya England alipata tatizo hilo Oktoba 30, wakati FC Barcelona ilipokuwa ikivaana na Alaves kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga).

Katika mchezo huo nyota huyo alilala chini na kushika kifua huku akieleza kuwa, alikuwa anashindwa kupumua lakini kwa sasa hali yake inaendelea vizuri na madaktari wamemtaka mchezaji huyo kupumzika kwa muda wa miezi mitatu.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Camp Nou, ulishuhudia wenyeji FC Barcelona ikipata sare ya 1-1, ambapo Mshambuliaji Memphis Depay aliifungia Barca dakika ya 49 na Luis Rioja aliisawazishia Alaves dakika ya 52.

Morrison: Tuwe pamoja naimani mambo yatakuwa vizuri
Mbeya Kwanza yamstaajabisha Malale Hamsini