Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally ameipiga kijembe Young Africans, kufuatia mapokezi makubwa iliyoyapata jana Jumapili (Juni 26), jijini Dar es salaam.

Kikosi cha Young Africans kilipokewa kishujaa na Wanachama na Mashabiki wa klabu hiyo kikitokea jijini Mbeya, ambako kilikabidhiwa Kombe la Ubingwa wa Tanzania Bara, baada ya mchezo dhidi ya Mbeya City FC.

Ahmed amesema hana budi kuipongeza Young Africans kwa mafanikio ya kutwaa Ubingwa wa Tanzania Bara, lakini anaamini kufurika kwa Mashabiki katika mapokezi ya timu yao, kumetokana na ukame wa miaka mitano ambayo ilishuhudia wakimaliza mikono mitupu.  

Amesema anaamini ingekuwa upande wa Simba SC, mapokezi yasingekua ya mafuriko kama ilivyokua jana Jumapili (Juni 26), kwani Mashabiki na Wanachama wao wameshazoea Ubingwa.

“Nawapongeza Yanga SC kwa kufurika, najua wamefurika kwa sababu wana ukame wa miaka mitano. Tungebeba sisi hata watu 20 usingewaona uwanja wa ndege maana tushazoea” Ahmed Ally

Young Africans imetwaa ubingwa wake wa kwanza baada ya kutoka kapa kwa misimu minne mfululizo, huku ikiaacha Simba SC patupu msimu huu.

Aliyejifungua mapacha wanne kuhamishiwa mjini
Ramadhan Kabwili aaga rasmi Young Africans