Mwanamke mmoja mfungwa nchini Vietnam amefanikiwa kukwepa hukumu ya kunyongwa iliyokuwa inamkabili baada ya kufanikisha zoezi la kujidunga ujauzito katika hali ambayo haikutarajiwa.

Maafisa wanne wa jeshi la magereza wamefukuzwa kazi kutokana na kisa hicho. Sio kwa kutuhumiwa kumpa ujauzito mwanamke huyo, la hasha! Bali kufanya uzembe ulimpa fursa mwanamke huyo kujidunga mimba yeye mwenyewe.

Mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina la Nguyen Thi Hue, 42, aliyefungwa katika gereza moja katika mkoa wa Quang Ninh, kaskazini mwa Vietnam, alitumia fursa ya sheria ya nchi hiyo inayozuia mwanamke mwenye ujauzito au aliye na mtoto wa chini ya umri wa miaka mitatu kunyongwa, na badala yake kupewa kifungo cha maisha.

Kwa mujibu wa gazeti la Thanh Nien News la nchini humo, Ninh alikamatwa mwaka 2012 kwa kosa la kuingiza madawa ya kulevya nchini humo na mahakama ilimhukumu adhabu ya kifo miaka miwili baadae.

Uchunguzi uliofanywa ulibaini kuwa mwanamke huyo alinunua mbegu za kiume kutoka kwa mfungwa mmoja mwenye umri wa miaka 27, na alimlipa kiasi cha $2,300 (sawa na shilingi 5,034,010 za Tanzania). Mwaamke huyo alitumia mbegu hizo kujidunga ujauzito.

Katika majaribio ya kufanikisha kupata ujauzito, imebainika kuwa mfungwa wa kiume alimpa mwanamke huyo mbegu zake mara mbili mwezi Agosti 2015.

Mwanamke huyo anatarajia kujifungua Aprili mwaka huu na tayari amebadilishiwa hukumu kutoka adhabu ya kunyongwa kuwa kifungo cha maisha.

 

Magufuli ageukia wasanii, aagiza TRA kufanya operesheni kama ya makontena
Uchaguzi Uganda: Museveni aeleza sababu za kuzima data, mawasiliano na huduma za kifedha