Meneja wa klabu ya Aston Villa, Tim Sherwood ameendelea kuweweseka kwa kuhofia kibarua chake huko Villa park, kufuatia mambo kuzidi kumuendelea hovyo.

Sherwood alishuhudia mwishoni mwa juma lililopita, kikosi chake kikishindwa kufanya vyema katika mchezo wa ligi ya nchini England dhidi ya Chelsea kwa kukubali kufungwa mabao mawili kwa sifuri.

Alipokutana na vyombo vya habari mara baada ya mchezo huo, meneja huyo kutoka nchini England, alikiri kikosi chake kupoteza muelekeo na kuahidi kusaka mbinu mbadala za kuwawezesha kufanya mazuri yanayokusudiwa.

Hata hivyo amerejea tena mpango wake kwa kusisitia jambo la kusaka mafanikio kwa kusema, hana budi kubuni njia tofauti za kusaka namna ya kupata point tatu kwa kuwaeleza wachezaji wake umuhimu wa kufanya linalokusidiwa viwanjani.

Amesema anajua yupo katika wakati mgumu, na wakati mwingine ameanza kusikia baadhi ya majina yakitajwa kwa kupewa nafasi ya kwanza kuchukua nafasi yake huko Villa Park.

Lakini alichokiahidi yeye ni kutohofia jambo hilo la kupoteza kazi, na badala yake kuendelea kufanya mikakati ya kufanikisha mambo yawe mazuri kwa kupata ushindi unaokusudiwa na walio wengi.

Mameneja wanaotajwa sana kuwa katika mipango ya kukaribia kupewa ajira huko Villa Park, kama mbadala wa Sherwood ni David Moyes pamoja na Brendan Roddgers.

Falcao Kutimka Chelsea
MIlner: Nina Imani Na Jurgen Klopp