Mshambuliaji kutoka nchini Burundi Amis Tambwe ana matumaini makubwa ya kuifunga Simba kwa kile alichosema kuwa watani wao hao ni wa kawaida kikubwa ni kuweka mipango mizuri.

Kinachompa jeuri hiyo Tambwe ni ukuta wa Simba aliodai kuwa ni mwepesi mno na hajaona beki yeyote wa kumzuia atakapokwenda kutikisa nyavu za wapinzani wao hao katika mechi yao itakayochezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

“Mabeki wa Simba ni wa kawaida sana tu na wanapitika, hivyo sina hofu na mechi hiyo, kikubwa timu ishinde bila kujali nani kafunga,” alisema Tambwe ambaye alisajiliwa Yanga akitokea Simba akiwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara na kuongeza

Hata hivyo, Tambwe amekiri kuwa kikosi cha Simba si kibaya hivyo mechi hiyo itakuwa ngumu na upinzani mkubwa.

“Hata sisi tuna mapungufu yetu, na wao wana mapungufu yao, inategemea nani atatumia vizuri makosa ya mwenzake, ila sisi tunajipanga vizuri kwa ajili ya kushinda hiyo mechi, ili kutangaza ubingwa mapema amesema,” alisema Tambwe.

Katika mzunguko wa kwanza Yanga ilishinda bao 2-0 na sasa wanajipanga kuhakikisha wanaendeleza ubabe huo ingawa Simba nao hawataki kukubali kuwa wateja wa Yanga huku wakiwa na hamu kubwa ya kushinda ili watwae ubingwa wa VPL.

Tayari Simba ipo kileleni kwa pointi 45 ikiwa ikecheza mechi 19 huki Yanga ikishika nafasi ya pili wakiwa wamekusanya pointi 43 na wamecheza mechi 18.

Ronaldo Ashangaza Kwenye Mkutano Na Waandishi Wa Habari
Azam FC Yazidi Kujiandaa Kisayansi Kombe La Shirikisho