Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania – KKKT, Askofu Dkt. Fredrick Shoo amesema suala la uwekezaji linaunga mkono na halipingwi kwani Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ana ni a na anahitaji Taifa la Tanzania kuwa na maendeleo.

Askofu Dkt. Fredrick Shoo, ameyasema hayo katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) katika Chuo cha Tumaini Makumira – Arusha hii leo Agosti 21, 2023, ambayo yamehudhuriwa na Mgeni rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Tunajua wewe kwenye nia yako unataka uwekezaji. Hata hivyo kumekuwa na maoni mbalimbali kwenye vyombo vya habari na mitandaoni tumeona maoni mbalimbali, sisi viongozi wa dini tuliomba kukuona na ulitupokea na kupokea pia maoni yetu kwa kupitia madhehebu yote nchini Tanzania. Tuna imani na wewe Mheshmiwa Rais.”

Aidha, Askofu Shoo pia amewaomba Viongozi wa dini kuacha tabia ya kuwagawa Watanzania kwa misingi ya kidini na kikabila na kwamba yeyote anayetaka kufanya hivyo, anapaswa kukemewa vikali na kuisihi Serikali iwakatae watu wanaotaka kufanya hivyo kwani hawana nia njema na Taifa.

Ufungaji wa Makanisa ni njama kuzuia Injili - Mchungaji Odero
KKKT inafanya kazi kwa ukaribu na BAKWATA - Injinia Kitundu