Kama ni mfuatiliaji mzuri au mhudhuriaji mzuri wa matamasha ya Bongo Flava, utagundua kuwa waimbaji karibu wote wakubwa hivi sasa wanawatumia wachezaji (ma-dancer) wanaong’arisha jukwaa, lakini hilo ni nadra sana kuliona kwa Barnaba.

Barnaba ambaye sauti yake na uwezo wake mkubwa wa kutunga na kuimba uliwa-inspire wasanii wakubwa kama Diamond Platinumz amesema kuwa yeye hahitaji kuwa na wachezaji/wanenguaji jukwaani kwasababu sauti yake na uwezo wake vinatosha kutoa burudani kali.

“Sauti yangu pekee yenyewe ni dancer,” Barnaba aliiambia XXL ya Clouds Fm. “Kitu kingine mimi sio mtu wa style hizo. Muziki wangu hauendani. Sio kama nakataa dancers, wakitokea nafanya lakini sio mtu wa kukaa na ma-dancer.”

Barnaba2

“I need to be International kwenye muziki wa Live. Mimi naimba Live. Ni mwanamuziki ambaye nimekamilika kwenye package ya mwanamuziki lakini sio kwenye kutumia dancers. Naweza kutumia dancers kwenye shows moja moja lakini sio zile corporate shows,” aliongeza.

Barnaba ameandika nyimbo kubwa na aliwahi kipaji chake kimeshawakuna wasanii wakubwa  Afrika waliomnyooshea mikono akiwemo Fally Ipupa wa Jamhuri ya Watu wa Kongo ambaye aliwahi kuimba naye.

TANZANIA KUWA MWENYEJI KONGAMANO LA MAJI AFRIKA
Justin Bieber aanzisha vita kali Instagram, ataka mashabiki wamsaidie