Kama ulikuwa hujui, kinachoandikwa na mitandao ya kijamii na tovuti mbalimbali duniani huwa na maana kubwa kwa wasanii wanaoandikwa na kuna wakati wengi wao hugeuka maadui wakubwa wa tovuti hizo kama ilivyokuwa kwa Justin Bieber.

Mwimbaji huyo ameanzisha vita kali dhidi ya tovuti maarufu ya habari za burudani ya Hollywoodlife akitaka kuiua kabisa kwa kile alichodai inaandika habari za uongo na zinazoumiza.

Kupitia Instagram, Bieber amewataka mashabiki wake zaidi ya milioni 71.6 wanaomfuata kumsaidia kupambana na tovuti hiyo hadi ifungwe kwa kuiripoti kama ‘Spam’ kwenye mitandao ya kijamii.

Ameanzisha pia kampeni maalum akitaka mashabiki wake (beliebers) kuiandika kwenye mitandao tuvuti hiyo kuwa ni ‘takataka’ kupitia hashtag #hollywoodlifeisgarbage. Mashabiki wake wamelianzisha na sasa Twitter imekuwa na hashtag hiyo maarufu iki-trend.

Hivi karibuni, Hollywoodlife imekuwa ikiripoti habari mbalimbali kuhusu Bieber na aliyekuwa mpenzi wake, Selena Gomez lakini ndani ya saa 24 tangu aanzishe vita hivyo dhidi yao ni kama wamemzira au wameachana naye.

A photo posted by Justin Bieber (@justinbieber) on

Barnaba awakacha ‘ma-dancer’
Video: Kim Kardashian afunika jarida la GQ kwa mara ya kwanza na picha ‘tata’