Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesimamisha shughuli zote za Benki M na kuiweka chini ya uangalizi wake kuanzia leo hii Agosti 2, 2018.
Benki Kuu imefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa Bank M inaupungufu mkubwa wa ukwasi kinyume na sheria ya mabenki na taasisi za kifedha ya mwaka 2006.
Hayo yamebainishwa na Gavana wa benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa kabla ya kuchukua maamuzi hayo benki hiyo iliongezewa muda wa mwezi mmoja ili iweze kukamilisha taratibu za mtaji lakini kwa bahati mbaya imeshindwa kufanya hivyo.
Aidha, Januari 4, 2018 BoT ilizipa miezi sita benki tatu ili ziweze kuongeza kiwango cha mtaji unaohitajika kutokana na matakwa ya kisheria ya kuwa na mtaji kamili wa kutosha.
-
JPM akerwa na jiji la Dar, sasa kuweka mkakati wa kushusha hadhi ya majiji
-
Video: Polisi wafunguka kuhusu kumkamata Zitto Kabwe, “Tunafanya kazi kwa weledi”
-
Video: Polisi wakanusha madai ya mbwa kupotea, ‘alikuwa masomoni’
Benki hizo ni Kilimanjaro Co-Operative Bank Limited, Tanzania Women Bank Plc na Tandahimba Community Bank Limited ambapo zilipaswa zitekeleze hayo kabla Juni 30, 2018