Serikali, imekemea vitendo vya utapeli vinavyoendelea kufanywa kupitia mitandao ya kijamii, dhidi ya wafanyabiashara wadogowadogo wenye kiu ya kujiondoa kwenye lindi la umasikini, kupitia taasisi za utoaji wa mikopo kwa njia ya mitandao nchini.

Kwa mujibu wa taarifa, iliyosambazwa kwa vyombo vya habari/mitandao ya kijamii na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imetoa ufafanuzi kwa umma kuhusu Kampuni inayoitwa Klynda E-Commerce Limited, baada ya kuona na kupokea malalamiko kuhusu uhalali wa biashara inayofanywa na kampuni hiyo.

Kampuni ya Klynda E-Commerce Limited, iliyosajiliwa Juni 14, 2022 na kupewa cheti cha usajili namba 1564483877 kwa ajili ya shughuli za uuzaji wa jumla wa vifaa vya kielektronic na mawasiliano, pamoja na ufanyaji wa biashara ya kiteknolojia ya kimataifa mtandaoni, imekuwa na taarifa zisizo rasmi zinazoleta taharuki kwenye jamii kwa kufanya biashara ya upatu ya kukusanya fedha kutoka kwa wananchi kwa ahadi ya kupata faida ndani ya muda mfupi kinyume na utaratibu.

Kutokana na Kampuni ya Klynda E-Commerce Limited, kudaiwa kwenda kinyume na utaratibu wa usajili BRELA imetoa angalizo kwa umma kuwa, kabla ya kuingia kwenye mahusiano ya kibiashara na kampuni yeyote, ni vema kupata uthibitisho wa uhalali wa uwepo wa kampuni hiyo pamoja na biashara husika, kupitia mamlaka za Serikali kwa kutembelea tovuti www.brela.go.tz

Taarifa hiyo, imeongeaza kuwa kumekuwa na matukio ya baadhi ya watu wasio waaminifu kughushi vyeti vya makampini, majina ya biashara na leseni za biashara kwa lengo ovu la kuwatapeli wananchi.

Hadi sasa, BRELA imebainika na kujiridhisha kuwa kampuni zilizosajiliwa kihalali kama Kopafasta Limited, Champion investiment na Afric zimekuwa zikitumiwa na matapeli kujipatia fedha kinyume na sheria na tayari taarifa za makampuni haya kutumiwa vibaya na matapeli zimeshafikishwa katika vyombo vya dola na utaratibu wa kuwasaka wahusika zinaendelea.

Baraza la Wafanyakazi lajadili usalama sehemu za kazi
DAR24 Team 'yanoa makali' Ufukweni