Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya, amesema kuwa siasa isiingizwe kwenye vita ya madawa ya kulevya na kusema viongozi wasimdanganye Rais Magufuli ili kujihakikishia vyeo vyao au nafasi zao katika uongozi.

Bulaya ametoa rai hiyo bungeni alipokuwa akichangia mjadala wa taarifa za kamati na kusema Rais anapaswa kuambiwa ukweli ili waweze kumsaidia kupambambana vyema na madawa ya kulevya.

“Tusifanye siasa kwenye vita hii ya madawa ya kulevya, tusimuongopee Rais kwa kutaka kuhakikisha vyeo vyetu tumwambie ukweli, ili kumsaidia Rais anapaswa kumteua kamishna wa hii tume maana tangu tulipopitisha sheria hiki chombo hakina kamishna, tutakapo hakikisha hicho chombo kinapata kamishna kwa kumsaidia Rais tutakamata wale wanaoingiza dawa za kulevya wale mapapa na si hao wanaokamatwa sasa hivi” amesema Bulaya
Mbali na hilo Mbunge huyo amesema kuwa hawa watu wanaokamatwa sasa hivi wanapaswa kupelekwa mahospitali kupata matibabu na si vinginevyo kwani hao ni waathirika wa dawa.

Amesema kuwa kama kweli Makonda akitaka kupambana na dawa za kulevya aende magerezani atakutana na kina mama Reyla watamwambia mapapa wa madawa ya kulevya, ili kuungana pamoja na kuhakikisha nchi inapambana vikali dhidi ya madawa ya kulevya.

Hany Abo Rida: Bado Tunamuhitaji Hector Cuper
Video: Meya atoa neno shule 6 zilizofanya vibaya matokeo kidato cha nne Dar