Waziri wa Nishati, January Makamba amesema endapo mradi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere Hydro Power project lilipo Mkoa Pwani, usingefiki hatua ya sasa ya ujazaji maji mikoa ya Pwani na Morogoro ingeathirika na mafuriko kama ilivyokuwa kwa msimu wa mwaka 2019/2020.
Makamba ameyasema hayo mara baada ya kufika kwenye mradi huo na kukagua hatua mbalimbali zinazoendelea kufanyika , na kuonesha kufurahishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo ambao kwa sasa umefikia asilimia 86.
Amesema “kabla ya Bwawa hilo kukamilika na kuanza rasmi kuzalisha umeme, tayari faida zimeanza kuonekana kwa Taifa katika siku mbili zilizopita maji yameingia mengi kuliko yale yaliyoleta mafuriko 2019/2020, neema iliyopo zile hatari za mafuriko ziko upande wa chini kwa maana hio hili bwawa limeanza kuzaa matunda yale tuliyokua tunayatarajia.”
Bwawa la Mwalimu Nyerere kwa sasa limehifadhi Maji kiasi cha Mita za ujazo Bilioni 6 sawa na asilimia 20 ya mahitaji ya mradi huo ambao ni mita za ujazo Bilioni 30.