Hatimaye Mahakama Kuu ya Kanda ya Ziwa leo imetoa uamuzi juu ya kesi iliyofunguliwa mahakamani hapo na baba mdogo wa marehemu Alphonce Mawazo, Mchungaji Charles Lugiko akisaidiwa na mawakili watatu wa Chadema kuomba mahakama ibatilishe amri ya Polisi kuzuia mwili wa mawazo kuagwa jijini humo.

Jaji Lameck Mlacha aliyekuwa akisiliza shauri hilo namba 11 ya mwaka 2015 amefuta amri ya Jeshi la Polisi na kutoa ruhusa kwa familia ya marehemu pamoja na wananchi kuendesha shughuliza kumuaga jijini Mwanza.

Aidha, Jaji Mlacha ameliagiza jeshi hilo kutoa ulinzi wa kutosha katika siku hiyo na kutahadharisha kuwa ulinzi huo uzivuke mipaka.

Katika hukumu hiyo, Mahakama imekaririwa ikisema kuwa ‘kazi ya jeshi la polisi ni kulinda raia na sio kuzuia mazishi.

Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza lilizuia shughuli za kuaga mwili wa Mawazo katika jiji hilo kwa kile walichodai kuwa kuna tishio la kipindupindu hivyo mikusanyiko hairuhusiwi jijini humo.

Alphonce Mawazo aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Geita na kiongozi wa Kanda ya Ziwa wa chama hicho. Pia aliwakuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chamdema. Aliuawa kikatili kwa kukatwa na panga na watu wasiojulikana mkoani Geita.

Serikali Yakata Mirija Mingine ya Matumizi
Kiongozi wa Kenya akwaa kashfa ya ufisadi kwa kuhudhuria sherehe ya Magufuli