Gavana wa Jimbo la Siaya nchini Kenya anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi na ibadhilifu wa fedha ya umma alizotumia kuhudhuria sherehe za kumuapisha rais John Magufuli, Novemba 5.

Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya hesabu za serikali nchini Kenya, Nicholas Gumbo amesema kuwa Gavana huyo aliitumia kiasi cha shilingi milioni 400 za Tanzania kama gharama za kuhudhuria sherehe hizo, kinyume cha taratibu.

Mwenyekiti huyo alihoji matumizi ya fedha hizo akidai ni ufisadi kwa kuwa sherehe hiyo haikuwa na uhusiano wowote na Maendeleo ya jimbo la Siaya kwa kuzingatia kuwa viongozi wa ngazi za juu zaidi walihudhuria.

“Sidhani kama Dk Magufuli ana uhusiano wowote na wananchi wa kaunti ya Siaya kiasi cha Gavana kutumia fedha hizo za umma kwenda Tanzania, “alisema Gumbo.

Hata hivyo, tuhuma hizo zilikanushwa vikali na Gavana Rasanga na kudai kuwa hazina ukweli kwani alihudhuria sherehe hizo kwa mwaliko binafsi wa Rais Magufuli.

“Hii ilikuwa safari binafsi. Hatukutumia fedha za serikali kama ilivyoelezwa,” alisema Rasanga na kupngeza kuwa mwenyekiti wa kama ya Bunge ya hesabu za serikali alitaka kujiinua kisiasa.

Rais Uhuru Kenyatta alihudhuria sherehe za kuapishwa kwa Dk Magufuli kuwa Rais wa serikali ya awamu ya Tano ya  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chanzo : Daily Nation

Chadema, Familia ya Mawazo yashinda Kesi dhidi ya Polisi, Mawazo Kuagwa Mwanza
Magufuli afuta sherehe Siku ya Ukimwi Duniani