Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli amefuta sherehe za maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani, Disemba Mosi.

Taarifa ya tamko la rais ilitolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue ambapo alieleza kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya sherehe katika maadhimisho hayo zitatumika kununua dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi, (ARV).

Tayari Tacaids wamewaagiza watendaji wake mikoa yote kusitisha maandalizi ya sherehe hizo badala yake wafuate maigizo ya Rais. 

Kaimu Mkurugenzi wa Mwitikio wa Taifa wa Tume ya kudhibiti Ukimwi (Tacaids) ameeleza kuwa siku hiyo watafanya kazi ya kutoa elimu kwa umma pamoja na takwimu lakini hakutakuwa na risala, hotuba, matembezi au vikundi vya burudani.

Kiongozi wa Kenya akwaa kashfa ya ufisadi kwa kuhudhuria sherehe ya Magufuli
Picha: IS Watoa Picha Ya Mtu Aliyelipua Gari La Walinzi Wa Rais Wa Tunisia