Mwananmuziki maarufu nchini marekani Christopher Maurice Brown maarufu kama Chris Brown ameripotiwa kuchunguzwa na Polisi mara baada ya mwanamke mmoja kudai kumshambuliwa kwa kupigwa nyumbani mjini Los Angeles.

Kwa mujibu wa Tovuti ya TMZ imeripoti kuwa mwanamke huyo amabye jina lake limehifadhiwa amefungua mashtaka akidai kuwa Breezy alimfanyia kitendo hicho nyumbani kwake mjini San Fernando Valley wikendi iliyopita.

Aliwaambia polisi kwamba Chris Brown alimchapa makofi ya nguvu kisogoni hadi kumtoa wigi lake, kimeeleza chombo hicho cha habari.

Hat hivyo mpaka sasa hakuna aliyekamatwa lakini mamlaka imethibitisha kwamba polisi walifika nyumbani kwa msanii huyo kufuatia tukio hilo linalodaiwa baada ya kutajwa kama mtuhumiwa katika ripoti ya polisi.

Kihongosi Katibu Mkuu mpya UVCCM
Hamisa, Samatta wateuliwa kuwa mabalozi uhamasishaji kulipa kodi