Bao lililofungwa na Mshambuliaji Raizin Hafidh limefuta mpango wa Pamba FC wa kushinda mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi Kuu hatua ya mtoano (Play Off).

Mchezo huo uliounguruma Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza ulishuhudia Coastal Union inayojitetea isishuke daraja ikipata bao la kuongoza dakika ya kwanza kupitia kwa Abdul Suleiman Sopu kabla ya James Ambrose hajaisawazishia Pamba FC na kufanya kipindi cha kwanza kumalizika kwa timu hizo kufungana bao 1-1.

Kipindi cha pili Pamba FC ilipata bao la pili kupitia kwa Emmanuel Hauled kwa mkwaju wa penati, lakini Raizin Hafidh akairejesha mchezoni Coastal Union na kuufanya mpambano huo kumalizika kwa sare ya 2-2.

Kabla ya mchezo huo kuanza majira ya saa kumi jioni, Wachezaji wa Coastal Union waligoma kuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo, kwa kuhofia imani za kishirikina.

Mchezo wa mkondo wa pili kwa timu hizo utapigwa Julai 24 Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga na matokeo ya jumla yataamua ima Coastal Union ibaki Ligi Kuu ama kushuka hadi Daraja la Kwanza, au Pamba FC ibaki Ligi Daraja la Kwanza au ipande Ligi Kuu msimu ujao 2021-22.

Mtibwa Sugar yatengeneza mazingira kubaki Ligi Kuu
CCM yampongeza mbunge Mabula kwa ziara yenye tija kwa wananchi