Daraja la Nyerere linalorahisisha usafiri wa wanaovuka kutoka kuelekea Kigamboni jijini Dar es Salaam limetajwa kuwa chanzo kingine kikubwa cha mapato jijini humo baada ya kuingiza shilingi bilioni 1.3.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Profesa Godius Kahyarara jana alieleza kuwa kiasi hicho cha fedha kimekusanywa tangu daraja hilo lilipofunguliwa rasmi, Mei 14 mwaka huu.

Alisema kuwa kiasi hicho cha fedha kinatokana na makusanyo ya magari, pikipiki na bajaji zilizopita katika daraja hilo katika kipindi hicho.

Naye Msimamizi wa mradi huo, Gerald Sondo ameeleza kuwa wamepanga kufanya maboresho makubwa katika mfumo wa kufanya malipo, ili wateja wao waweze kufanya malipo kwa kutumia kadi ya kielektroniki. Hatua hiyo imeonakana kuwa itapunguza kwa kiasi kikubwa msongamano wa magari unaoonekana hasa wakati wa sikukuu.

“Tunatarajia kuanzisha mfumo wa malipo kwa kutumia kadi za kielektroniki ambapo madereva wa vyombo vya usafiri watakuwa wanatumia kulipa tozo pindi wanapopita darajani,” alisema.

Kwa mujibu wa uongozi wa daraja hilo, vyombo vya moto vya usafiri vinavyopita katika daraja hilo kwa siku ni kati ya 8,000 hadi 10,000.

Daktari feki aliyetinga ICU Awekwa kati
Picha: Mabingwa Wa Euro 2016 Wapokelewa Kishujaa