Nyota wa muziki kutoka nchini Nigeria David Adedeji Adeleke maarufu Davido ametangaza neema kwa raia wa nchini Nigeria kwa kuamua kugawa kiasi cha pesa kisichopungua Naira Milioni 20 ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni 111 za Kitanzania.

Pesa hizo atazigawa kwa takriban watu ishirini ambao kila mmoja atapata kiasi cha Naira milion 1, ambazo ni sawa na Milioni 5.5 za Kitanzania.

Davidi amedai kuwa anaitoa kama mtaji au kianzio kwa wananchi wa Nigeria watakaomtumia mawazo na mikakati yao ya biashara, na watakaokuwa na mipango mizuri dio watakaoshinda na kupata kitita hicho.

Davido ameutumia ukurasa wake wa mtandao wa twitter kubainisha hilo, huku akieleza kuwa anaona serikali ya nchini Nigeria imeshindwa kuwasaidia raia wake kujiinua.

Mchakato wa kugawa pesa hizo umepangwa kufanyika mapema machi 18, 2022, ambapo mpaka sasa inaelezwa kuwa Davido ameanza kupokea mawazo ya biashara kutoka kwa watu mbali mbali wakisubiri wakati ambao mwanamuziki huyo ataanza kuwataja rasmi washindi.

Simon Msuva: Haki itafuata mkondo wake
Saido Ntibazonkiza kuikacha Young Africans?