Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo ametembelea baadhi ya shule wilayani humo kukagua ujenzi wa madarasa na mwitikio wa wanafunzi kuripoti shuleni.

Akizungumza baada ya kukagua shule mbili za sekondari Ndalala na Karibuni, Jokate amesema ameridhishwa na ujenzi wa madarasa, na kuwezesha wanafunzi wote kuingia shule kwa wakati

Aidha ametoa rai kwa walimu wa shule hiyo kuendelea kufundisha kwa weledi ili kuzalisha wataalamu wengi zaidi.

Pia Jokate ametoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha ujenzi wa madarasa 157 wilayani humo.

“Kwa kweli ujenzi wa madarasa 157 haijawahi kutokea kwa wakati mmoja, ni mradi ambao pia tumeukamilisha ndani ya muda mfupi na matokeo yake nadhani leo mmeyaona,”Amesema Jokate.

Tarehe 17 Januari 2022, wanafunzi wamerejea shuleni baada ya likizo ya mwisho wa mwaka huku Rais Samia Suluhu akitatua kwa kiwango kikubwa uhaba wa madarasa nchi nzima.

Waziri Mkuu awataka mabalozi kuvutia wawekezaji
TMA: Mvua kubwa kunyesha kwa siku tatu