Diamond Platinumz ameweka wazi kilichojili hadi kufikia hatua ya kuwapeleka wasanii wa label yake ya WCB nyumbani kwa Rais mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete.

Wiki kadhaa zilizopita, Diamond na uongozi wake pamoja na wasanii wa kundi hilo walionekana katika picha kadhaa wakifanya mazungumzo na Dk. Kikwete na Mkewe Mama Salma, nyumbani kwake.

Diamond ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa kwa muda mrefu alipanga kukutana na Dk. Kikwete kwakuwa alikuwa na mambo ya kujadili naye kutokana na fursa alizozipata nchini Marekani hivi karibuni, lakini pia aliiona hiyo kuwa ni fursa ya kuitambulisha kwake WCB.

“Unajua kwa muda mrefu nilipanga kukutana naye lakini alikuwa bize sana, kwahiyo alipopata muda aliniita nyumbani kwake nikaona ni vyema niende na WCB,” alisema Diamond.

“Lakini kuna vitu pia nilitaka kuongea naye kwa sababu nilipokuwa Marekani kuna vitu nilikuwa nimevipata nilitaka kuzungumza naye tuone jinsi ya kufanya,” aliongeza.

Dk. Kikwete alikuwa kiongozi aliyekuwa karibu na wasanii wa Bongo Flava, na kwamujibu wa Diamond Platinumz siku moja alitembelea Ikulu na kubaini kuwa picha yake ni miongoni mwa picha za wasanii zilizokuwa zimebandikwa ndani ya Makao hayo ya Mkuu wa nchi.

Uganda wafanya mashindano ya ‘Miss & Mr HIV/AIDS’
Video: Jaji Mutungi anaivuruga CUF - Mbowe