Imefahamika kuwa Uongozi wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans umepanga kuanza mazungumzo na Mlinda Lango chaguo la Kwanza Djigui Diara kwa ajili ya kumsainisha Mkataba Mpya.

Mlinda Lango huyo kutoka nchini Mali amekua chagizo la Mafanikio ya Kikosi cha Young Africans tangu aliposajiliwa Klabuni hapo, mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Stade Malien ya nchini kwao.

Taarifa zilizopatikana kutoka ndani ya Young Africans zinaeleza kuwa, Uongozi wa juu umepanga kumsainisha Mkataba mpya Kipa huyo kabla ya kufikia mwishoni mwa msimu huu 2022/22, kufuatia kuvutiwa na uwezo wake.

“Uongozi hautaki kumuachia mchezaji yoyote aliye kwenye kiwango bora kwa sasa, lengo kubwa ni kutengeza timu bora itakayoendelea kufanya vizuri katika Michuano ya Ndani na Nje ya Nchi.”

“Tayari baadhi ya wachezaji ambao mikataba yao itafikia tamati mwishoni mwa msimu huu wameanza mazungumzo na wengine wameshasaini mikataba mpya.”

“Miongoni mwao ni Wakongomani Yanick Bangala na Djuma Shaban, ambao wametupa ubingwa msimu uliopita na tunaamini msimu huu wataendelea kutoa mchango wa kutupa mafanikio katika Ligi ya Ndani na Michuano ya Kimataifa.” amesema mtoa taarifa kutoka Young Africans

Hivi karibuni Rais wa Young Africans Hersi Said aliwahi kukaririwa na baadhi ya Vyombo vya Habari akisema hawatamuachia mchezaji yoyote wanayemuhitaji kuondoka na badala yake watamuongezea mkataba kwa lengo la kutengeneza timu imara na bora.

Tisa wanaswa na dawa za kulevya Dar
Kocha wa viungo kutangazwa Simba SC