Michuano ya klabu bingwa Ulaya hatua ya makundi inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi usiku wa leo huku michezo minane ikipigwa katika viwanja mbalimbali.

Katika michezo ya kundi H Borussia Dortmund watawakaribisha mabingwa watetezi wa kombe la klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid katika uwanja wa Signal-Iduna-Park huko Urarumani wakati Apoel Nicosia ikicheza dhidi ya Tottenham.

Kundi E – Sevila inacheza na Maribor, Spartak Moscow dhidi ya Liverpool, Kundi F – Manchester city inacheza na Shakhtar Donetsk, Napoli inacheza na Feyenoord na Kundi G- Besiktas inacheza na Rasen Ballsport , Monaco dhidi ya FC Porto.

Kesho Jumatano Kundi A – FC Basel itacheza na Benfica, CSKA Moscow na Manchester United. Kundi- B Anderlecht dhidi ya Celtic, PSG itakwaruzana na Bayern Munich.

Kundi C- Qarabag dhidi ya As Roma, Atletico Madrid wanakutana na Chelsea, Kundi – D Juventus itacheza na Olympiacos huku Sporting ikichuana na Barcelona.

Rihanna ataja wacheza soka anaowakubali, atamani kuolewa nao
Peter aivunjavunja Psquare, ajiita Mr.P