Mshambuliaji hatari wa Man Utd, Wayne Rooney ameamua kuelekea Dubai kupumzika huku akiuguza jeraha ya mguu wake wa kulia ambalo limemuweka nje ya uwanja kwa sasa.

Rooney, ambaye huenda akashindwa kuonekana tena uwanjani mpaka mwishoni mwa mwezi huu, amefunga safari hiyo kwa kuamini akifanya hivyo huenda ikawa wepesi kwake kujifariji kufuatia jeraha ambalo limemnyima nafasi ya kuitetea klabu yake ya Man Utd ambayo inahaha kumaliza katika nafasi nne za juu.

ronnry32

Picha za mitandao ya kijamii, zimemuonyesha mshambuliaji huyo akiwa katika eneo la maonyeho ya wanyama huko Dubai, ikiwa ni sehemu ya mapumziko yake ambayo yamepewa baraka zote na meneja wa Man Utd, Louis Van Gaal.

Inasemakana Rooney, amefikia kwenye chumba cha hotel exlusive ambapo analipa kiasi karibia shilingi za kitanzania 3,000,000 kwa siku, huku akitegemewa kurudi kwenye kikosi cha United mwishoni mwa mwezi huu.

ronnry3

Hata hivyo, Rooney anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya England ambacho kitakwenda nchini Ufaransa kupambana kwenye fainali za mataifa ya barani Ulaya (Euro 2016) zitakazoanza mwezi June mwaka huu.

Msimu huu Rooney ameonyesha kuhangaika sana katika mbinu zake za kutikisa nyavu za timu pinzani, tofauti na ilivyokua katika misimu kadhaa iliyopita, hali ambayo ilianza kuibua hofu na mashaka kwa mashabiki wake, ambapo hata hivyo walianza kurishishwa naye kutokana kasi yake kuanza kurejea taratibu kabla hajaumia mguu mwezi uliopita.

Massimiliano Allegri Avunja Ukimya
Jux aweka wazi mtego uliotumika kunasa penzi la Vanessa Mdee, ni ‘kadude’