Bondia Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ ameibuka na kumtangazia hali ya hatari mpinzani wake kutoka DR Congo Tshimanga Katompa kuelekea pambano lao la Julai 15, jijini Dodoma chini ya Kampuni ya Peak Time Media.

Dullah Mbabe amesema amedhamiria kushinda pambano hilo, ili kulipa kisasi cha kupigwa katika pambano lililomkutanisha na Bondia huyo miaka miwili iliyopita.

Bondia huyo amesema kilichotokea katika pambano lililopita hadi kufikia hatua ya kupoteza, ilitokana na yeye kuwa amechoka baada ya kupigwa na Twaha Kiduku ambapo Katompa kwa kumwambia kuwa safari kazi atakuwa nayo kwa kuwa amekuwa fiti zaidi.

Ikumbukwe Dullah Mbabe mwaka juzi akipoteza kwa kipigo kibaya mbele ya Katompa kutoka DR Congo katika pambano ambalo lilivunja utawala wake wa muda mrefu hali iliopelekea anaonekane bondia wa kawaida.

Mbabe amesema kuwa Katompa aliweza kumpiga kirahisi kwa kuwa tayari alikuwa amemkuta amechoka baada ya pambano lake na Twaha Kiduku hivyo anatakiwa ajipange kuelekea katika pambano lake la marudiano litakalopigwa Julai 15, mwaka huu jijini Dar.

“Mashabiki wangu wanatakiwa wajue kwamba Katompa alinipiga kwa sababu alinikuta nimetoka kwenye mechi ngumu dhidi ya Twaha Kiduku ambayo Kiduku mwenyewe alikuwa amebebwa kwa sababu nilimtandika ngumi kali iliopelekea ahisabiwe lakini hakuweza kuhesabiwa.

“Lakini nataka nimwambie kwamba Dullah wa sasa siyo yule wa zamani ambaye yeye anaona aliweza kumtandika kirahisi, nimejipanga vya kutosha yaani safari hii hataki atapigwa anataka atapigwa kutokana na maandalizi makubwa ambayo naendelea kuyafanya juu yake,” amesema Dullah.

Polisi yathibitisha vifo watu watano ajali ya Coaster na Lori
Ajali ya Basi dogo na Lori Mikumi: Watano wahofiwa kufa