Kocha wa Simba Muingereza Dylan Kerr amesema kuwa beki wa timu hiyo Ramadhani Kessy yupo huru kufungasha virago na kutafuta timu nyingine kama atashindwa kukubaliana na timu hiyo.

Mkataba wa sasa wa Kessy na Simba umebakia miezi sita ambapo anaruhusiwa kufanya mazungumzo na timu yoyote na amekuwa akisitasita kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Kerr alisema kuwa beki wake Mrundi, Emery Nimubona, ambaye naye anacheza namba moja na Kessy, ameanza kuonyesha kiwango kizuri, hivyo hana wasiwasi hata akiondoka.

“Kama Kessy anataka kuondoka aende zake tu, kwani hata akiondoka halitakuwa jambo la kuiumiza sana Simba, kwa sasa beki wetu Emiry (Nimubona) ameanza kunifurahisha, anacheza vizuri sana tofauti na zamani.

“Leo (juzi) nimeamua kumuanzisha ili nimuangalie kama kweli atafaa kuziba pengo la Kessy kama akiondoka na nimeona kweli anaweza, hivyo niwatoe wasiwasi mashabiki wa Simba, hata akiondoka mrithi wake tunaye,” alisema Kerr.

Yaya Toure: Soka Haikua Ndoto Yangu
UEFA Kuchezesha Droo Ya Champions League Leo