Nchi za Argentina, Chile, Paraguay na Uruguay kwa pamoja zimewasilisha rasmi maombi/zabuni ya ya kutaka kuwa wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia 2030.

Nchi hizo nne za Amerika Kusini zimetoa wito kwa Kombe la Dunia kurudi kule ambako soka ilizaliwa. Mashindano hayo yalifanyika kwa mara ya kwanza katika mji mkuu wa Uruguay, Montevideo mwaka 1930.

Rais wa Shirikisho la soka la Amerika Kusini ‘COMNEBOL’ Alejandro Dominguez amesema kuwa “Kombe la dunia 2030 linastahili kusheherekewa kipekee kwani itakuwa imetimia miaka 100 tangu kuanza kwa mashindano hayo”.

“Tunaamini FIFA inao wajibu wa kuipa heshima kumbukumbu ya wale waliotangulia kuyaamini na kuyaanzisha mashindano haya”.

Baada ya Fainali za 2022 kumalizika nchini Qatar, Maandalizi ya Fainali za Kombe la Dunia 2026 yameanza rasmi katika nchi za Marekani, Canada na Mexico.

Wahandisi GGML wafanya ziara ya mafunzo Darajani
Tetemeko Uturuki, Syria: Idadi ya vifo yafikia 9,504