Uongozi wa shirikisho la soka duniani FIFA, kesho utakutana na wadhamini wakuu waliokubali kufanya biashara na shirikisho hilo, kwa lengo la kufahamu mustakabali wa mambo yatakavyoendeshwa kwa kipindi cha miaka kadhaa ijayo.

Mkutano huo wa pande hizo mbili unafanyika kwa mara ya kwanza, baada ya kuibuka kwa kashfa iliyowahusha baadhi ya maafisa wa FIFA, waliokua wanajipatia fedha kwa njia za udanganyifu.

Katibu mkuu wa FIFA, Jerome Valcke amesema mkutano huo utafanyika mjini Zurich, yalipo makao makuu ya shirikisho hilo.

Valcke, amesema mkutano huo utafanyika baada ya ombi lililowasilishwa na maafisa wa makampuni ya Coca-Cola, Visa pamoja na McDonald ambao watakua na mengi ya kuzungumza ili kufahamu ni vipi watakavyoweza kuendelea kufanya mipango ya biashara.

Makampuni hayo ambayo yamekua na uhusiano mzuri na FIFA kwa miaka kadhaa, yalionyesha kushtushwa na kashfa iliyoibuka ndani ya shirikisho hilo miezi mitatu iliyopita, ambapo shirika la upepelezi la nchini Marekani FBI lililazimika kuwatia nguvuni baadhi ya maafisa waliobainika kujihusha na vitendo vya kuomba mlungula.

Nape Amshambulia Lowassa Kivingine
Maradona Amzawadia Muamuzi Wa Mkono Wa Mungu