Beki wa kati kutoka nchini Brazil na klabu ya Arsenal, Gabriel Armando de Abreu Paulista, amefutiwa adhabu ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa wakati wa mchezo wa ligi ya nchini England mwishoni mwa juma lililopita.

Chama cha soka nchini England FA, kemefikia maamuzi ya kumfutia adhabu beki huyo mwenye umri wa miaka 24, baada ya kupokea na kuipitia rufaa iliyowasilishwa na viongozi wa klabu ya Arsenal mara baada ya mchezo wa siku ya jumamosi.

Imedhihirika Paulista hakufanya kosa la kujaribu kumpiga kwa nyuma Diego Costa, kama ilivyoeleweka kwa muamuzi Mike Dean.

FA wamebaini Costa alimuhadaa muamuzi huyo kwa kumshurutisha amuadhibu Paulista kwa kigezo cha kupigwa kwa nyuma, hali ambayo imechukuliwa kama makossa ya kibinaadamu yaliyofanywa na Mike Dean.

Paulista, alistahili kukosa michezo mitatu iliyo chini ya chama cha soka nchini Engalnd FA kutokana na adhabu iliyomkumba wakati wa mchezo dhidi ya Chelsea, na sasa anakua huru.

Angelina Jolie Na Brad Pitt Waongeza Mtoto Kutoka Syria
Diego Costa Ahukumiwa Kwa Kosa La Kupiga