Kocha wa muda wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate ameutaka uongozi wa chama cha soka nchini humo FA, kumuweka wazi kuhusu suala la ajira.

Southgate ametoa muda wa mwezi mmoja kwa viongozi wa FA kwa kuamini utakua wakati sahihi kwao kufanya maamuzi ya mustakabali wake, na kama itakua kwa mtu mwingine atakua tayari kumuachia majukumu.

Kocha huyo ambaye alipewa jukumu la kukaa kwenye benchi la timu ya taifa ya England, baada ya kujiuzulu kwa Sam Allardyce mwezi wa tisa mwaka huu, ametoa muda huo alipozungumza na vyombo vya habari kuelekea mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Hispania ambao utachezwa kesho jijini London.

Mbali na kuwa kocha wa muda wa timu ya taifa ya England, pia Southgate mwenye umri wa miaka 46 ni mkuu wa benchi la ufundi la timu ya taifa ya vijana ya nchi hiyo chini ya umri wa miaka 21.

“litakua jambo zuri kwangu kufahamu mustakabli wa kazi ninayoifanya kwa sasa, naamini mpaka mwezi ujao FA watakua wameshatoa jibu sahihi,” Alisema.

“Tunakabiliwa na changamoto ya kuiwezesha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21, ili ifuzu fainali za Ulaya, na kwa sasa nina jukumu lingine la kuisaidia timu ya taifa ya wakubwa katika michezo ya kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018, ni vyema nikafahamu wapi ninapostahili kupatumikia kikamilifu.” Aliongeza Southgate

Mohamed Salah, Abdallah Saied Waizima Ghana
Trump: Wahamiaji haramu jiandaeni kuondoka