Ahadi za wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi zimezua mengi katika mchakato wa kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu huku kila mgombea akijitahidi kutafuta namna ya kuwahakikishia wananchi kuwa  atatekeleza kweli alichoahidi.

Mgombea urais wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Hamad Rashid Mohamed amewaahidi wananchi wa Zanzibar kuwa endapo watamchagua kuwa rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar atahakikisha anawakomboa wananchi kutoka kwenye umasikini na kuwa na maisha ya kipato cha kati.

Katika kuonesha kuwa ana uhakika na ahadi yake hiyo, Hamad Rashid ambaye ni mbunge wa Wawi, amewaambia wananchi kuwa endapo atapewa nafasi ya kuongoza serikali hiyo kwa muhula mmoja wa miaka 5 na akashindwa kutekeleza ahadi hiyo, atajisalimisha mwenyewe gerezani na kutumikia kifungo cha miezi sita.

Hamad Rashid aliongeza kuwa kwa kuwa anauhakika wa kutekeleza ahadi yake, ameamua kujitoa kwa ajili ya kujiadhibu kama hatatekeleza na kwamba anatoa wito kwa wanasiasa wenzake wanaotoa ahadi mbalimbali kuthubutu kusema kama alivyosema yeye.

Hamad Rashid Mohamed alihamia katika chama cha ADC baada ya kuondoka katika Chama Cha Wananchi (CUF), huku akipewa kadi namba 1 ya chama hicho hali iliyoibua hisia kuwa ndiye mmiliki wa chama hicho.

Wenger Arudisha Majibu Kwa Mourinho
Platini Kuwania Kiti Cha Urais Wa FIFA