Dereva wa timu ya Mercedes, Lewis Hamiliton ameongeza wigo wa alama kati yake na mpinzani wake, Sebastian Vettel kutoka timu ya  Ferrari baada ya kuongoza kwenye mbio za leo Singapore Grand Prix

Hamiliton ameongoza mbio hizo mwanzoni kabisa baada ya Sebastian Vettel kugongana na dereva mwenzake wa Ferrari, Kimi Raikkonen pamoja na Max Verstappen wa Red Bull na kumuacha Hamiliton akiongoza mbio hizo hadi mwisho.

Aidha, Vettel na wenzake walijitoa baada ya kugongana hivyo inawabidi wasubiri mbio zinazokuja ili kuona kama wanaweza kumpiku Hamiliton katika nafasi yake hiyo anayoishikilia.

Hata hivyo, Mbio za leo za SingaporeGP zimefanyika usiku kwa mara ya kwanza katika historia ya Formula1, ambapo Lewis Hamiliton kwa sasa amejiongezea pointi 25 ambazo zinamfanya kufikisha pointi 263 dhidi ya 235 za Sebastian Vettel

Wahukumiwa kwenda jela miaka 35
Mbunge Musukuma akamatwa na Polisi