Kiungo Henrikh Mkhitaryan amesema hana uhakika kama atakua fit kabla ya mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England ambao utashuhudia klabu yake ya Man Utd ikiwakabirisha Man City kwenye uwanja wa Old Trafford mwishoni mwa juma hili.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, alilazimika kurejea Old Trafford mwishoni mwa juma lililopita akitokea kwenye kambi ya timu ya taifa lake la Armenia, baada ya kuumia paja la mguu wa kulia wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Jamuhuri Ya Czech.

Hatua hiyo ilimsababishia Mkhitaryan kukosa mchezo wa kuwania kucheza fainali za kombe la dunia kati ya Armenia dhidi ya Denmark uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita.

Mkhitaryan ambaye alijiunga na klabu ya Man Utd miezi mitatu iliyopita akitokea Borussia Dortmund kwa ada ya Pauni milioni 26, ameandika katika ukurasa wake wa Instagram “Ninaendelea na matibabu, lakini sina uhakika kama nitakua fit kwa ajili ya mchezo wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Man City,”

“Ninahamasika kufanya jitihada za kurejea katika hali yangu ya kawaida, kutokana na kupenda kuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza soka dhidi ya Man City siku hiyo, lakini bado nina mashaka makubwa ya kutimiza malengo hayo!

“Ninawashukuru kwa kuendelea kunionyesha upendo na kunipa ushirikiano.” Ameandika Mkhitaryan akielekeza ujumbe huo kwa mashabiki wake

Makamu wa Rais akanusha kutaka kujiuzulu
Video: Kama bado unatumia simu feki kwa matumizi mengine, Serikali imetoa maelezo haya