Jina lake halisi ni Emilio Stanley Mwai Kibaki lakini aliijulikana zaidi kama Mwai Kibaki.

Alizaliwa 15/11/1931 kaunti ya Nyeri, na kubatizwa mwaka 1932 na padri Mmisionari wa kanisa takatifu katoliki la mitume.

Alipewa jina Emilio linatokana na neno la Kilatini ‘Aemilius’ yani mtu mpambanaji (rival).

Alikua kipanga shuleni. Alihitimu kidato cha nne 1950 na kupata alama A ktk masomo yote 6.

Mwaka 1951 alijiandikisha kujiunga na jeshi lakini Gavana Walter Coutts alipiga marufuku waKikuyu, waEmbu na waMeru kujiunga na jeshi, hivyo akapoteza nafasi.

Mwaka 1952 alijiunga na Chuo kikuu Makerere na kuhitimu mwaka 1955, shahada ya Uchumi (First Class Honours, BA Economics).

Mwaka 1956 aliajiriwa kama Meneja msaidizi wa masoko kampuni ya mafuta ya Shell nchini Uganda.

Baadae alipata scholarship London School of Economics kusoma Shahada ya umahiri ya usimamizi wa fedha (MSc in public finance).

Mwaka 1958 alirudi Makerere kama Mhadhiri msaidizi (Assistant Lecturer).

Mwaka 1960 aliitwa Kenya na aliyekua Katibu Mkuu wa KANU, Tom Mboya kusaidia harakati za kudai uhuru.

Mwaka 1963 alichaguliwa Mbunge wa jimbo la Donholm (kwa sasa linaitwa Makadara), kisha akateuliwa Naibu waziri wa Fedha.

Mwaka 1964 aliteuliwa Waziri wa viwanda na biashara.

Mwaka 1969 akateuliwa Waziri wa fedha.

Mwaka 1978 akawa Makamu wa Rais, chini ya utawala wa Moi.

Mwaka 1988 akaondolewa Umakamu wa Rais na kuteuliwa Waziri wa Afya.

Baada ya mfumo wa vyama vingi, alijiondoa KANU na kujiunga na chama cha upinzani cha DP.

Mwaka 1992 aligombea Urais kwa mara ya kwanza akashindwa. Mwaka 1997 akagombea kwa mara ya pili akashindwa. Mwaka 2002 akagombea kupitia muungano wa vyma vya upinzani (NARC) akashinda, na kuondoa utawala wa KANU uliodumu kwa miaka 40.

Mwaka 2002 alishinda Urais akiwa mgombea wa upinzani na mwaka 2013 akaachia Urais kwa mgombea wa Upinzani.

Sarafu ya shilingi 40 ya Kenya ina taswira yake.

Ameacha watoto watano. Wanne wa ndoa (Judy, Jimmy, David na Tony) na mmoja wa nje ya ndoa (Wangui) aliyezaa na mbunge wa Othaya, Mary Wambui.

Kwaheri Emilio. Kwaheri “the rival” till we meet again.!

Mwai Kibaki kuzikwa Aprili 30
TANZIA: Mwai Kibaki afariki dunia