Rasmi Kiungo Mshambuliaji Ibrahim Ajib Migomba ameachana na Azam FC katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili msimu huu 2022/23.

Kiungo huyo ameondoka Azam FC baada ya kudumu kwa mwaka mmoja, ambao haukuwa na mafanikio ya kucheza katika kikosi cha kwanza, baada ya kuachwa na Simba SC Wakati wa Dirisha Dogo msimu uliopita 2021/22.

Azam FC imethibitisha kuondoka kwa Kiungo huyo Mzawa kwa kuweka taarifa Rasmi katika Kurasa zake za Kijamii ikiandika: #ThankYou Ahsante sana, Ibrahim Ajibu, kwa kuwa sehemu ya familia yetu.

Hata hivyo Taarifa za awali zinadai kuwa, Ajibu amesajiliwa Singida Big Stars na ataanza kuondoka kwenye kikosi cha Klabu hiyo baada ya taratibu zote za uhamisho kukamilishwa na Klabu hiyo ya Mkoani Singida.

Endapo Taarifa za Ajibu kusajiliwa Singida Big Stars zitathibitisha na Uongozi wa Klabu hiyo, bado Mchezaji huyo atajiunga na Wachezaji wengine ambao waliwahi kufanya nao Kazi kwenye klabu ya Simba SC.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Desemba 21, 2022
Juma Mgunda atanguliza heshima Kagera Sugar