Klabu ya Inter Milan inatajwa kuwa kwenye mpango wa kuwasajili wachezaji Mattia Zaccagni ambaye anapewa kipaumbele zaidi, na mlinda mlango Marco Silvestri kutoka Hellas Verona.

Inter Milan inajipanga kusawajili wawili hao wakati wa dirisha dogo la Usajili ambalo rasmi litafunguliwa juma lijalo, na wanaamini wachezaji hao wataweza kuongeza nguvu kwenye kikosi chao ambacho msimu huu kina dhamira ya kutwaa taji la Italia.

Zaccagni mwenye miaka 25, ni zao la kituo cha kukuza na kuendeleza vipaji kwa vijana chama Hellas Verona na mpaka sasa ameshafunga mabao matatu na kusaidia upatikanaji wa mabao 14 ya klabu hiyo.

Mlinda mlango Silvestri anahitajika mjini Milan kama chaguo la pili, lakini pia atakuwa mrithi wa nahodha wa sasa wa inter Milan Samir Handanovic.

Hata hivyo Inter Milan wamejipanga kutumia gharama nafuu, ambayo haitazidi Euro milioni 10, japo wachezjai hao wote mikataba minono ndani ya kikosi cha Hellas Verona.

Katika kuhakikisha wanatimiza lengo walilojiwekea, Inter Mipan wamejipanga kuwaingiza sokoni kwa makubaliano ya uhamisho wa mkopo Federico Dimarco na Eddie Salcedo.

Federiko amewekewa dau la Euro milioni 4.5, huku Salcedo akiwekwa sokoni kwa Euro milioni 10.

Polisi Tabora yawakamata 683
Mauaji ya waandishi wa habari yaongezeka

Comments

comments