Aliyewahi kuwa Mwanamuziki nchini Tanzania na mke wa Marehemu Regnald Mengi aliyekuwa mwenyekiti wa IPP, Jacqueline Mengi maarufu kama K-Lyinn amedai kuzuiwa kuingia kwenye kaburi la mumewe.
Kupitia ukurasa wake wa tweeter amebainisha kuwa amekuwa akifukuzwa yeye pamoja na watoto wake kwenye kaburi la marehemu mumewe jambo ambalo ameamua kuto likalia kimya.
“Nimenyamaza kwa mengi sana tu mmefikia hatua ya kunizuia mimi na wanangu kuingia kwenye kaburi la mume wangu.”
“Tunafukuzwa eti mpaka tuombe ruhusa ya kuingia kwenye kaburi la mume na Baba wa watoto wangu. Nimechoka, sitakubali kuendelea kuona wanangu wakisononeka na sitakaa kimya.”ameandika Jacqueline Mengi.
Ikumbukwe kuwa Reginald Mengi ambaye alikuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP alifariki dunia Mei 2, 2019 na kuacha mke (Jacqueline Mengi) na watoto watano ambao ni Regina, Rodnay, Abdiel, Jayde na Ryan. Watoto hao amezaa na Mercy Mengi pamoja Jackline Mengi.