Mtendajji mkuu wa klabu ya Bayer Leverkusen  Rudi Voller amelegeza kamba kuhusu mpango wa kukubali kumuachia mshambuliaji kutoka nchini Mexico Javier Hernández Balcázar Chicharito.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, amekua katika rada za klabu za nchini Hispania Sevilla CF na Valencia FC, na inaelezwa huenda akahamishwa wakati wa dirisha dogo la usajili (Mwezi januari mwaka 2017).

“Tunataka kufanya maamuzi kwa njia ya amani, tunatoa nafasi kwa yoyote kuzungumza nasi kuhusu Chicharito ili tuachacne na taarifa za vyombo vya habari, kila jambo lina wakati wake na hatutotaka kuliendea haraka’

“Chicharito ni mchezaji ambaye huwezi kuzuia hisia zake kama anataka kubaki ama kuondoka tutafahamu wakati utakapofika, hivyo tutakua tayari kuzungumza na yoyote atakaekuja na ofa nzuri.

“Chicharito bado ana mkataba na Bayer Leverkusen  hadi mwaka 2018. Na ninahisi hata wanaopanga kumsajili wanalifahamu jambo hili.”  Voller ameliambia jarida la BILD.

Pluijm Ataja Sababu Za Kumuweka Benchi Ali Mustapha ‘Barthez’
Samir Nasri Afichua Siri Ya Kuondoka Etihad Stadium