Baadhi ya wanachama wa Simba SC, wamemtwisha mzigo wa lawama msemaji wa Yanga, Jerry Muro kuwa ndiye chanzo cha kuboronga katika baadhi ya mechi zao, ikiwa bado wanakuna kidonda cha kipigo cha Toto Africans ya Mwanza.

Akiongea na Uhuru Fm, mwenyekiti wa tawi la Simba la Mpira Pesa, maarufu kwa jina la ‘Ustadh’ amedai kuwa maneno ya Muro yanadhihirisha kuwa anaihujumu timu hiyo na ndio chanzo cha wao kushindwa hasa katika mechi yao dhidi ya Toto Africans.

Alisema kuwa wao wanashangaa kuona Jerry Muro akisema wanafungwa, wanafungwa kweli huku wachezaji wao wakionesha uzembe katika baadhi ya maeneo hivyo wanaamini huwa wananunuliwa kupitia Msemaji huyo wa Yanga.

“Inawezekana tunahangaika lakini kumbe kuna wachezaji wetu ambao wanapokea mshahara mara mbili ili kutuhujumu,” alisema.

Jana Simba ilikubali kipigo cha 1-0 kutoka kwa Toto Africans ambao wanaaminika kuwa ni ndugu wa karibu wa wapinzani wao, Young Africans.

Baada ya Mchezo huo, mashabiki wa Simba walifanya tukio la ‘aibu’ kwa kufanya vurugu na kuyashambulia kwa baadhi ya wachezaji na viongozi wa klabu hiyo. Hali iliyopeleka polisi kuingilia kati na kuwatawanya kwa mabomu ya machozi.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), limelaani vikali kitendo hicho na kuvitaka vyombo vya usalama kuchukua hatua dhidi ya mashabiki waliohusika kwani kufanya fujo ni kosa la jinai.

Mtuhumiwa Kesi ya Kutoa lugha chafu dhidi ya Rais Magufuli atoka Rumande
Mkuu wa Wilaya amtaka Waziri Nchemba kutokanyaga kijijini kwake