Kiungo wa klabu ya Rangers ya Scotland Joey Barton anakabiliwa na adhabu kwa kucheza kamari kinyume na sheria za soka nchini humo.

Barton anatuhumiwa na chama cha soka nchini Scotland (SFA) kwa kuweka dau mara 44 kati ya Julai 1 na Septemba 15 mwaka huu.

Barton atarejea katika klabu hiyo baada ya kufungiwa kwa muda wa majuma matatu kutokana na tukio hilo ambalo limetafsiriwa kama utovu wa nidhamu.

SFA kupitia sheria yake kifungu cha 33 inakataza wachezaji, makocha, maofisa wa klabu na waaamuzi nchini humo kuweka dau kuhusu matokeo ya michezo popote pale duniani.

Mwezi May, kiungo wa Partick Thistle Steven Lawless alifungiwa michezo 6 baada ya kuthibitika alicheza kamari ya michezo 513.

 

NEC na ZEC zakutana kubadilishana uzoefu
Santi Cazorla: Bado Ninaipenda Arsenal FC